Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-USALAMA

Jeshi la Sudan kusini lataka uchunguzi ufanyike kufuatia kuibuka kwa uhasama

Jeshi la Serikali ya Sudan Kusini limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa ukiukwaji wa makubaliano yaliyosianiwa hivi karibuni ili kukomesha mashambulizi ya vita nchini Sudan Kusini huku likinyooshea kidole cha lawama upinzani kwa kushambulia ngome zake.

Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017, wakiomba vita visitishwe.
Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017, wakiomba vita visitishwe. STEFANIE GLINSKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Masaa kadhaa baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kibinadamu ya kusitisha uhasama huko Addis Ababa Ethiopia Alhamisi Disemba 21 kundi la SPLA-IO linaloongozwa na Riek Machar na vikosi vya serikali vilishambuliana katika ngome zao nchini kote.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa SPLA Brigedia Generali Lulu Ruai Koang alitoa taarifa ya kushutumu waasi kwa kufanya mashambulizi kwenye ngome za majeshi ya serikali katika majimbo matano ambayo ni Mto Yei, Liech Kaskazini, Amadi, Awiel Mashariki na Fashoda, ndani ya saa 24 hadi 72.

Koang amesema waasi hao walifanya operesheni dhidi ya SPLA kwa lengo la kupata maeneo mapya ya kimkakati kabla ya wachunguzi wa amani wa IGAD kuzuru nchini humo

Kufuatia hatua hiyo Koang ametoa wito kwa jumuiya ya IGAD kutuma haraka wachunguzi na waangalizi wa amani kuchunguza suala hilo sambamba na kuweka na kuhakiki ni nani kwa sasa wako katika udhibiti wa maeneo yote yaliyoshambuliwa na waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.