Pata taarifa kuu
DRCONGO

Wafungwa 19 watoroka gerezani Kalehe DRC

Wafungwa kumi na tisa, wengi wao wanaokabiliwa na mashtaka ya ubakaji, wametoroka jela mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo usiku wa kuamkia leo, na kusababisha hofu ya kulipiza kisasi kwa waathirika wa vitendo vyao, vyanzo vya serikali za ndani vimesema.

Moja ya tundu lililotumiwa na wafungwa kutoroka kwenye gereza la Kinshasa Mwezi Mei.
Moja ya tundu lililotumiwa na wafungwa kutoroka kwenye gereza la Kinshasa Mwezi Mei. DRC
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msimamizi wa gereza Gerard Nkwana, katika jimbo la Kivu Kusini Wafungwa hao 19 walitoroka katika gereza la Kalehe lenye wafungwa 20.

Pascal Nabulera, mkuu wa shirika la kijamii jamii la Kalehe, amesema,Watu wanaofika mahakamani kufungua kesi na mashahidi sasa wanawasiwasi wa kulipiziwa kisasi na wafungwa hao waliotoroka.

Nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yenye umasikini na inayopambana na mgawanyiko wa kisiasa na kikabila pamoja na machafuko mashariki mwa nchi inakabiliwa na matatizo makubwa katika mfumo wake wa mahakama.

Mnamo Mei, wafungwa 4,000 walitoroka katika gereza la Makala huko Kinshasa, mji mkuu, wakati 900 wakitoroka kutoka jela huko Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.