Pata taarifa kuu
DRC-MAANDAMANO-USALAMA

Upinzani wa Rassemblement waitisha maandamano dhidi ya Kabila

Muungano wa Upinzani wa Rassemblement nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umeitisha maandamano ya nchi nzima hivi leo kumshinikiza rais Jospeh Kabila kuondoka madarakani kufikia mwisho wa mwaka huu.

Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Rassemblement, Felix Tshisekedi.
Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Rassemblement, Felix Tshisekedi. REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Upinzani pia unataka kuwepo kwa serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Mwenyekiti wa muungano huo Felix Tshisekedi pia ametupilia mbali mswada wa sheria za uchaguzi na kusema kuwa zinahatarisha mchakato mzima na wakati huo huo kuwataka wananchi wajitokeze kwa uwingi kuhishiriki maandamano ya hii leo.

Hata hivyo serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano hayo ikisema kuwa ni kutokana na sababu za kiusalama.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.

Polisi jijini Kinshasa katika siku zilizopita, wamekuwa wakikabiliana na waandamanaji wa upinzani kwa kuwakamata na hata kuwafwatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi.

Watu kadhaa walikamatwa na wengine kujeruhiwa katika mandamano yaliyofanyika hivi karibuni katika miji ya Goma na Bukavu, mashariki mwa DRC, kumshinikiza rais Kabila ajiuzulu kabla ya tarehe 30 Desemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.