Pata taarifa kuu
CAMEROON-HAKI-USALAMA

Watu zaidi ya 10 wapoteza maisha katika maandamano Cameroon

Hali ya sintofahamu ilishuhudiwa siku ya Jumapili Oktoba 1 katika mikoa ya watu wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon. Wanaharakati wanaotaka kujitawala kwa mikoa hiyo walitangaza kwamba wafuasi wao wamekuwa wakiandamana takriban mwaka sasa kwa kile wanachosema kubaguliwa katika mfumo wa elimu na sheria.

Polisi wa Cameroon wakipiga doria katika mtaa wa Buea tarehe 1 Oktoba, 2017.
Polisi wa Cameroon wakipiga doria katika mtaa wa Buea tarehe 1 Oktoba, 2017. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano na vikosi vya usalama yalizuka katika maeneo kadhaa ya watu wanaozungumza Kiingereza.Inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa katika makabiliano hayo lakini taarifa hii haijathibitishwa mpaka sasa.

Kwa upande wa waandamanaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo hayo, kazi ilikuwa ngumu kuliko ilivyotarajiwa. Walitakiwa kutumia mbinu zaidi kutokana na wingi wa polisi na askari waliokua walitumwa kuzingira maeneo hayo ya Kusini-Magharibi na Kaskazini Magharibi.

Wakati nmwingine, walikabiliana na vikosi vya usalama, walipokua wakijaribu kuvunja vizuizi vya polisi, hususan kusini-magharibi kwenye kituo cha usafiri kkaribu na mji wa Limbe, ambapo makabiliano mkali yalishuhudiwa. Kwa mujibu wa mashahidi, baadi ya waandamanaji walivamia kituo cha polisi.

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika makabiliano hayo haijajulikana. Picha kadhaa za watu waliopoteza maisha zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, bila hata hivyo kujua mazingira halisi ya vifo vyao.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Rais wa Cameroon, Paul Biya amelaani ghasia zilizotekelezwa na pande zote baada ya polisi kuwapiga risasi na kuwauwa zaidi ya watu kumi wakati wa maandamano hayo.

Ghasia hizo zimetokea wakati wa maadhimisho ya miaka miaka hamsini na sita tangu kujumuishwa kwa jimbo la wazungumzaji wa Kiingereza ndani ya Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.