Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRCONGO

Kituo cha radio chafungiwa Burundi kwa kukosoa serikali

Kituo CCIB FM+ cha radio nchini Burundi kimefungiwa kwa muda baada ya kukosoa serikali kufuatia mauaji ya warundi wakimbizi nchini Jamuhuri ya demokrasia ya Congo.

Willy Nyamitwe, Waziri wa mambo ya kigeni wa Burundi
Willy Nyamitwe, Waziri wa mambo ya kigeni wa Burundi Photo : RFI / Richard Riffonneau
Matangazo ya kibiashara

CCIB FM+, cha nchini Burundi mapema mwezi huu kilitoa taarifa za kukosoa mwenendo wa serikali baada ya mauaji ya warundi 36 katika maandamano ya sept 15 nchini Drc ambayo pia askari mmoja wa Drc aliuawa.

Mkurugenzi na muhariri Eddy Claude Nininahazwe aliiambia AFP kuwa kituo kimezuiwa kwa kutangaza ukimya wa serikali baada ya mauaji ya warundi.

Katika taarifa ya serikali baraza la habari lilidai kituo hiko kimefanya ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya habari na sheria zinazosimamia vyombo vya habari na kukiamuru kuzima mitambo yake kwa miezi mitatu kuanzia jumatatu.

Nininahazwe amelaani hatua hiyo akijitetea kituo chake hakikuvunja sheria yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.