Pata taarifa kuu
DRC-UN

Raisi Kabila aahidi uchaguzi wa DRC kufanyika

Raisi wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema kuwa taifa lake linaelekea katika uchaguzi huku akijiapiza kupingana na mashinikizo ya kigeni katika kuandaa kalenda ya uchaguzi huo wa kihistoria.

Raisi wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akihutubia mkutano wa Umoja wa mataifa UN nchini Marekani
Raisi wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akihutubia mkutano wa Umoja wa mataifa UN nchini Marekani REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Marekani Kabila ametoa wito kwa marafiki wa DRC kumuunga mkono katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kiusalama wakati taifa hilo linapoandaa uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa rfi mjini New York kabla ya hotuba yake raisi wa DRC Joseph Kabila alikutana na raisi wa umoja wa Afrika Alpha Conde, waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel,mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda na kamishna mkuu wa haki za binadamu Zeid Al Hussein.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na makundi ya upinzani mwaka jana uchaguzi unapaswa kufanyika mwaka huu katika taifa hilo na kupisha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya demokrasia nchini DRCongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.