Pata taarifa kuu
DRC-BURUND-MAUAJI-USALAMA

Mauaji ya Warundi Kamanyola: Marekani na Umoja wa Ulaya walionya jeshi la DRC

Marekani na Umoja wa Ulaya wamelionya jeshi la jamuhiri ya kidemorasia ya Congo kututmia nguvu kubwa baada ya kutokea kwa mauaji ya wakimbizi wa Burundi wapatao 39 mashariki mwa nchi hiyo.

Mji wa  Kamanyola, mashariki mwa DRC, ambapo jeshi liliwaua kwa kuwapiga risasi wakimbizi 37 kutoka Burundi.
Mji wa Kamanyola, mashariki mwa DRC, ambapo jeshi liliwaua kwa kuwapiga risasi wakimbizi 37 kutoka Burundi. Latifa Mouaoued/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliotolewa na wiraza ya mambo ya nje ya Marekani imesema serikali ya Marekani imeguswa na matumizi ya nguvu yaliotumiwa na jeshi la DRCongo katika kuwatuliza wakimbizi Burundi huko Kamanyola, hali iliosababisha mauaji ya watu 39 akiwemo afisaa mmoja wa jeshi la FARDC.

Washington imeitaka serikali ya DRCongo kushirikiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi, pamoja na wanajeshi walinzi wa Amani wa Umoja Mataifa katika kurejesha uwiano baina ya wakimbizi na wananchi wakaazi wa maeneo jirani na kambi za wakimbizi.

Katika taarifa iliotolewa awali na umoja wa Ulaya jijini Kinshasa imevitaka vikosi vya jeshi la Congo kutumia weledi na sheria za kimataifa na kwamba uchunguzi lazima ufanyike ili kubaini wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Watu 36 waliuawa papo hapo mjini Kamanyola kwa kupigwa risase na jeshi la Congo lilipojaribu kuzima maandamano ya wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakidai kuachiwa huru kwa wenzao wawili waliokuwa wameshiikiliwa tayari kurejeshwa Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.