Makala hii imeangazia mkutano wa umoja wa mataifa ambapo viongozi wa dunia wanakutana kujadili juu ya namna ya kufikia utatuzi wa migogoro duniani, wakati huu Korea Kasakzini na Marekani zikivutana kuhusu silaha za nyuklia na majaribio ya makombora ya Pyongyang, mgogoro wa kidiplomasia kati ya mataifa ya uarabuni na Qatar, vita ya Syria, wakati kwenye barani Afrika, kule Burundi na maswala ya haki za binadamu yakiendelea, nchini DRC na swala la Uchaguzi,na mambo mengine.Katika makala hii utawasikia wachambuzi wetu Hamduni Marcel akiwa Mwanza, na Abdulkarim Atiki kutoka Daresalaam.