Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Minusma yalengwa na mashambulizi mawili mabaya

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali ililengwa na mashambulizi mawili siku ya Jumatatu Agosti 14. Shambulio la kwanza lilifanyika katikati mwa nchi, katika eneo la Douentza, shambulio la pili liliendeshwa kaskazini magharibi, katika mji wa Timbuktu.

Gari ya kijeshi ya Minusma, Timbuktu, Septemba 19, 2016.
Gari ya kijeshi ya Minusma, Timbuktu, Septemba 19, 2016. SEBASTIEN RIEUSSEC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kaskazini magharibi mwa Mali, watu wanaoshukiwa kuwa magaidi (wanne hadi sita, kulingana na vyanzo mbali mbali) wakati mwengine walisafirishwa kwa gari. Watu hao waliokua walijihami kwa mabomu na silaha za kivita, walitembea kwa miguu kwenye maeno ambayo yalionekana ni vigumu kwa gari kutumia barabara. Baada ya kuwasili katika makao makuu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa katika mji wa Timbuktu,walianza kuwafyatulia risase walinzi wa usalama wa kampuni binafsi inayofanya kazi kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma). Walinzi sita wa usalama waliuawa.

Washambuliaji wawili walifaulu kuingia ndani ya kambi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (Minusma) kwa kutumia silaha zao. Hata hivyo waliuawa na vikosi vya Minusma. Inaarifiwa kuwa askari kadhaa wa kikosi hiki cha Umoja wa Mataifa walijeruhiwa, huku mmoja akiwa akiwa katia hali mbaya. Vikosi vya jeshi la Mali pia viliingilia kati na kuweza kuwaua magaidi wengine.

Watu wawili wauawa katika eneo la Mopti

Mapema siku ya Jumatatu, katikati mwa Mali, katika mji wa Douentza, makao makuu ya ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, yalishambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi. Katika shambulio hilo askari mmoja wa Minusma na askari wa Mali waliuawa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulizi hayo.

Matukio haya yanatokea siku moja baada ya mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Burkina Faso. Kwa kuonyesha mshikamano wake na wananchi wa Burkina Faso, Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta anazuru Jumanne hii mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.