Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mashambulizi ya makundi yenye silaha yaongezeka DRC

Hali ya usalama inaendelea kutisha ikiwa ni pamoja kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi ya waasi katika wiki za hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkoa wa Kivu Kaskazini unakabiliwa na mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha (picha ya zamani).
Mkoa wa Kivu Kaskazini unakabiliwa na mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha (picha ya zamani). Antoine Sanfuentes/NBC NewsWire/Getty
Matangazo ya kibiashara

Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mji wa Beni ulikuwa ulikumbwa kwanza mapigano kati ya jeshi na makundi yenye silaha na kisha Rutshuru, na sasa wilaya ya Lubero inaendelea kukumbwa na mapigano hayo.

Mwishoni mwa wiki hii iliopita, mkoa wa Kivu Kusini ulikumbwa na mapigano, ambapo waasi walidhibiti vijiji kadhaa. Mapigano hayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu hamsinikwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu. Miongoni mwa waliopotezamaisha katika mapigano hayo ni hasa askari wa jeshi la DR Congo na raia kadhaa.

Mkoa wa Kivu ya Kusini ulishuhudiwa mapigano makali mwishoni mwa wiki hii iliopita. Katika mapigano hayo, mji wa Fizi, eneo lenye dhahabu nyingi ambapo waasi waliweza kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa ya mji huo na walifanya "mikutano ya hadhara na wakaazi wa vijiji hivyo ambapo waliwaomba wakaazi hao kutorudi kulipa kodi na kwa askari kujisalimisha.

Wakati huo jeshi DR Congo ilipelekaidadi kubwa askari ili kuendesha mashambulizi dhidi ya waasi hao. Hadi siku ya Jumatatu, vijiji vya Misisi na Lulimbavilikua bado mikono mwa waasi.

Polisi inalengwa na waasi

Katika maeneo kadhaa ya wilaya ya Lubero mkoani Kivu Kaskazini, wakaazi walisalia nyumbani siku ya Jumatatu wakipinga dhidi ya ukosefu wa usalama na kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi ya Mai Mai.

Itafahamika kwamba siku ya Jumamosi Makundi haya ya Mai Mai yalimteka "Kamanda wa polisi katika eneo la Kipese" kabla ya kurejea siku moja baadae na kuchoma ofisi zote za serikali, ikiwa ni pamoja na kituo cha polisi, ambapo waliwafungua wafungwa wengi.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mashambulizi ya makundi ya Mai Mai yameongezeka. Makundi hayo yanaendesha harakati zao katika maeneo yote ya machifu, ameonya mkuu wa wilaya ya Lubero.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.