Pata taarifa kuu
ALGERIA-MOROCCO-SYRIA-WAKIMBIZI

Algeria yamtaka balozi wa Morocco kutengua kauli yake kuhusu wakimbizi wa Syria

Wizara ya Mambo ya nje ya Algeria imemtaka Balozi wa Moroco nchini humo kukanusha madai kuwa Algiers iliwafukuza wakimbizi 55 kutoka Syria.

Vita nchini Syria imesanbabisha maelfu ya raia kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi mbalimbali.
Vita nchini Syria imesanbabisha maelfu ya raia kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi mbalimbali. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Algeria inasema madai hayo hayana ukweli wowote na yanalenga kulichafulia jina.

Kutokana na mzozo nchini mwao, baadhi ya raia wa Syria wamekuwa wakikimbilia kwenda nchini Morocco kupata hifadhi.

Machafuko nchini Syria yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kulazimika kuyahama makazi yao, na kukimbilia katika nchi mbalimbali duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.