Pata taarifa kuu
MALI-USALAM

Kambi ya kijeshi ya Gourma Rharous yashambuliwa na magaidi

Mashambulizi mabaya yalitokea siku ya Jumanne Aprili 18 katika kambi ya kijeshi mkoani wa Timbuktu nchini Mali. Idadi iliyotolewa na maafisa wa usalama inaeleza vifo vya askari wanne, wengine 16 walijeruhiwa. Kikosi cha jeshi la Ufaransa nchini Mali Barkhane kiliendesha operesheni dhidi ya na ugaidi ya tukio hiulo, na kuua watu kadhaa.

Kikosi cha askari wa Ufaransa waliwadhibiti magaidi ambao walishambulia kambi ya kijeshi ya Gourma Rharous, Mali.
Kikosi cha askari wa Ufaransa waliwadhibiti magaidi ambao walishambulia kambi ya kijeshi ya Gourma Rharous, Mali. © RFI/David Baché
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha askari wa Ufaransa, Barkhane, kilifaulu kuwakamata magaidi kwenye zaidi kilomita thelathini. Majeshi ya Ufaransayalitumia helikopta zao na kutangaza kuwaua magaidi wengi walio kuwa katika magari yao mawili madogo, ambapo walikua walijihami kwa silaha za kivita. Wakati huo huo magari mawili yaliibwa siku ya Jumanne asubuhi April 18 katika mashambulizi dhidi ya Gourma ya Rharous kambi.

Katika mashambulizi hayo ya kigaidi, askari wengi wa Mali walipoteza maisha, watu wengine kadhaa walijeruhiwa.Washambuliaji walichukua kila kitu walichokua wakiweza kubeba na kuchoma vilivyosalia baada ya mapigano makali.

Umoja wa Mataifa ulituma haraka helikopta zakekatika katika eneo hilo, lakini walipofika, washambuliaji walikuwa tayari wameshaondoka. Wakati huo huo kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane ndio waliingilia kati na kufaulu kukamata magaidi hao

Mashambulizi yalidaiwa kutekelezwa siku ya Jumanne jioni na muungano mpya wa wanajihadi unaodai kutetea "Uislamu na Waislamu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.