Pata taarifa kuu
DRC

Upinzani nchini DRC waitisha mgomo kushinikiza utekelezwaji wa mkataba wa kisiasa

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umeitisha mgomo wa kitaifa hivi leo kushinikiza utekelezwaji wa mkataba wa kisiasa uliotiwia saini kati yao na serikali mwezi Desemba mwaka 2016.

Jiji kuu la DRC Kinshasa, usalama umeimarishwa kwa hofu ya kutokea kwa ghasia
Jiji kuu la DRC Kinshasa, usalama umeimarishwa kwa hofu ya kutokea kwa ghasia REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa muungano huo wa Rassemblement, wakiongozwa na chama kikuu cha  UDPS, wanamlaumu rais Joseph Kabila kwa kutoonesha nia ya kutekeleza mkataba huo utakaounda serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu.

Wafanyikazi wa serikali na wale kutoka sekta za kibinafsi wametakiwa kusalia nyumbani siku ya Jumatatu kuonesha masikitiko yao kuhusu utekelezwaji wa mkataba huo na kuunga mkono jitihada za upinzani.

Ikulu ya rais Kabila kupitia ukurasa wake wa Twitter, imesema kiongozi huyo anatarajiwa kukutana na makundi mbalimbali ya kisiasa na mashirika ya kiraia siku ya Jumatatu na Jumanne kuona namna ya kutekeleza mkataba huo.

Shinikizo hizi zinakuja baada ya wasuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini humo ambao ni Maaskofu wa Kanisa Katoliki kuonesha masikitiko yao wiki iliyopita na kutangaza kujiondoa katika mchakato huo kwa kile walichokisema wanasiasa hawaoneshi nia ya kuutekeleza mkataba huo.

Ripoti zinasema kuwa mambo yote kuhusu utekelezwaji wa mkataba huo yamekamilika lakini utata unasalia kuhusu uteuzi wa Waziri Mkuu.

Upande wa serikali unataka upinzani kupendekeza majina matatu ili rais Kabila kuteua jina moja, lakini upinzani unataka kupendekeza jina moja ili kushikilia wadhifa huo.

Duru zinaeleza kuwa, upinzani untaka Felix Tshisekedi mtoto wa Ettiene Tshisekedi aliyekuwa kiongozi wa muungano huo kuwa Waziri Mkuu, suala ambalo pia limeugawa upinzani.

Tshisekedi alifariki dunia mwezi Februari akiwa jijini Ubelgiji na bado hajazikwa kwa sababu ya mvutano huu wa kisiasa.

Upinzani unasema kiongozi wao wa zamani atazikwa tu pale serikali ya mpito ikapoundwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.