Pata taarifa kuu
DRC-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano makali yazuka katika mji wa Mwene Ditu

Kumeripotiwa mapigano makali katika mji wa Mwene Ditu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mamia ya wananchi wamelazimika kukimbia makazi yao, hali ambayo imezua wasiwasi mkuwa eneo hilo.

Mkoa wa Kasaiya Kati, DRC unakabiliwa na ghasia tangu Agosti 2016.
Mkoa wa Kasaiya Kati, DRC unakabiliwa na ghasia tangu Agosti 2016. Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ujumbe wa serikali ya DRC umewasili katika mji wa Kananga jimboni Kasai ya Kati siku ya Jumapili usiku kujaribu kuzuia uasi unaofanywa na wapiganaji walio watiifu kwa kiongozi wa jadi katika jimbo hilo Kamuina Nsapu.

Kwa upande wao watu wa familia ya kiongozi huyo wa jadi katika jimbo hilo wameelezea wasiwasi wao na kubaini kwamba hali si shwari katika mji wao.

Jeshi la serikali ya DRC limekuwa likikabiliana na kundi la wapiganaji la BDK walio tiifu kwa kiongozi huyo Kamuina Nsapu katika jimbo hilo tangu kuuawa kwake mnamo mwezi Ogasti mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.