Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-MAZISHI

Mvutano waendelea kujitokeza kuhusu mahali atazikwa Tshisekedi nchini DRC

Ni takribani majuma mawili sasa toka kutokea kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi wa Mulumba, wanasiasa nchini humo wanaendelea kuvutana kuhusu mahali kiongozi huyo atazikwa, mwili wake utakapowasili.

Jeneza la Etienne Tshisekedi chini ya ulinzi mkali mjini Brussels, nchini Ubelgiji Januari 5, 2017.
Jeneza la Etienne Tshisekedi chini ya ulinzi mkali mjini Brussels, nchini Ubelgiji Januari 5, 2017. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Awali mwili wa Tshisekedi, ulikuwa uwasili jijini Kinshasa mwishoni mwa juma, lakini haikuwa hivyo baada ya chama chake cha UDPS, kudai kuwa mwili wake hauwezi kuingia nchini humo ikiwa utekelezwaji wa makubaliano ya Januari Mosi mwaka huu hayajatekelezwa.

Hata hivyo msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende, anaona kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya mazishi ya Tshisekedi na hali ya siasa ya nchi hiyo.

Mvutano huu huenda ukachelewesha zaidi kurejeshwa kwa mwili wa Tshisekedi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya mazishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.