Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-MOROCCO-USHIRIKIANO

Morocco kufadhili kuhamishwa kwa mji mkuu wa Sudan Kusini

Serikali ya Morocco imetangaza kuwa, itaisaidia Sudan Kusini kuhamishia mji mkuu wake kutoka Juba hadi Ramciel. Wakati huo huo Serikali ya Sudan Kusini na Umoja wa Mataifa wamekubaliana kuimarisha uhusiano wao.

Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, katika mji wa Juba, Februari 2, 2017.
Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, katika mji wa Juba, Februari 2, 2017. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Mfalme wa Morocco Mohamed wa Sita ambaye anazuru Juba kwa siku tatu, amesema kuwa serikali yake itatoa Dola za Marekani Milioni 5 kuanza ujenzi wa jiji kuu jipya.

Mwaka 2011, serikali ya Sudan Kusini ilitangaza mpango wa kuhamisha mji wake mkuu kwenda katika jimbo la Lakes.

Wakati huo huo Sudan Kusini na Umoja wa Mataifa, zimekubaliana kuimarisha uhusiano wao na kufanya kazi pamoja.

Hatua hii inakuja baada ya Juba, wakati wa Katibu Mkuu wa zamani Ban Ki Moon kushtumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Mwakilishi wa Umoja huo nchini humo David Shearer amesema Katibu Mkuu Antonio Guteres yuko tayari kuimarisha uhusiano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.