Pata taarifa kuu
GHANA-UCHAGUZI

Nana Akufo Ado kuapishwa leo nchini Ghana

Nana Akufo Ado anataraji kuapishwa hii leo kuwa raisi mpya wa Ghana baada ya kumshinda raisi anayemaliza muda wake John Dramani Mahama Katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Nana Akufo-Addo raisi mteule wa Ghana
Nana Akufo-Addo raisi mteule wa Ghana REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Ado mwenye umri wa miaka 72,Wakili wa zamani wa masuala ya haki za binadamu ataapishwa katika viwanja vya uhuru jijini Accra katika hafla itakayohudhuriwa na viongozi na umma usiopungua watu elfu sita.

Baadhi ya wakuu wa mataifa 11 kutoka barani Afrika wanataraji kuhudhuria akiwemo raisi anayemaliza muda wake na viongozi wa zamani John Rawlings na John Kufuor.

Jeshi la polisi katika jiji kuu la Accra limejiapiza kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea shughuli hizo za kula kiapo kwa raisi mpya ambapo barabara zinazoingia na kutoka zitafungwa kwa muda.

Wafanyabiashara wamejipanga kufanya biashara kwa kiwango kikubwa jirani na uwanja utakaokusanya umati utakaoshuhudia sherehe hizo.

Ushindi wa Akufo-Addo na makabidhiano ya amnai ya madaraka yanaiweka Ghana katika nafasi nzuri ya mfano wa demokrasia katika ukanda.

Muangalizi mmoja wa kimataifa ameielezea demokrasia ya Ghana kuwa ni ya kiwango cha Dhahabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.