Pata taarifa kuu
KENYA-AU

Rais Kenyatta amnadi Waziri Amina Mohammed kuwa Mwenyekiti mpya wa AU

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaomba viongozi wenzake barani Afrika kumuunga mkono Waziri wake wa Mambo ya nje Amina Mohammed, kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, AU.

Rais Uhuru Kenyatta akiwa na Waziri wake wa Mambo ya nje Amina Mohammed wakiwa mjini Marrakech Morroco Novemba 16 2016 walikohudhuria mkutano wa Mabadiliko ya hali ya hewa
Rais Uhuru Kenyatta akiwa na Waziri wake wa Mambo ya nje Amina Mohammed wakiwa mjini Marrakech Morroco Novemba 16 2016 walikohudhuria mkutano wa Mabadiliko ya hali ya hewa PHOTO | PSCU
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano jioni, pembezoni mwa mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa unaoendelea nchini Morocco, rais Kenyatta alikutana na marais 20 kutoka mataifa mbalimbali kuomba uungwaji mkono huo.

Miongoni mwa marais waliokutana na Kenyatta ni wale kutoka nchini Nigeria, Gabon, Rwanda, Ushelisheli, Visiwa wa Comoros, Sudan, Senegal na Chad.

Mbali na rais Kenyatta, naibu wake William Ruto na Mabalozi wengine wametembelea nchi 35 kumnadi Waziri Amina kupata kazi hiyo wakati wa mkutano wa marais utakaofanyika mwezi Januari mwakani jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Waziri Amina anatarajiwa kupambana na wagombea wengine wawili; Waziri wa Mambo ya nje kutoka Botswana Pelonomi Venson Moitoi, na Agapito Mba Mokuy, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje kutoka Equatorial Guinea.

Tayari Somalia na Misri, zimetangaza wazi kuwa zitamuunga mkono Waziri Amina kuchukua nafasi hiyo lakini matafa mengine ya Afrika uzoefu umeonesha wazi kuwa huwa yanapiga kura kwa makubaliano kutoka miungano wanayotoka kama kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC na ECOWAS.

Jaribio la kumtafuta kiongozi mpya wa AU atakayechukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma kutoka Afrika Kusini ambaye anastaafu baada ya kuhudumu kuanzia mwaka 2012, halikufanikiwa mwezi Julai jijini Kigali nchini Rwanda.

Uganda iliondoa jina la aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe aliyekuwa anatafuta nafasi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.