Pata taarifa kuu
UNICEF

Unicef: Wasichana wanatumia muda zaidi kufanya kazi za nyumbani kuliko wavulana

Wasichana wanatumia asilimia 40 zaidi ya muda wao kufanya kazi za nyumbani zisizokuwa na malipo ukilinganisha na wavulana, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na watoto, Unicef.

Msichana mdogo akionekana akiwa amebeba beseni za maji, inakadiriwa wasichana milioni 10 barani Afrika wanafanya kazi zisizo na malipo.
Msichana mdogo akionekana akiwa amebeba beseni za maji, inakadiriwa wasichana milioni 10 barani Afrika wanafanya kazi zisizo na malipo. UN Photo/Eskinder Debebe
Matangazo ya kibiashara

Unicef inasema kuwa, tofauti iliyopo ya muda wa kufanya kazi ni sawa na saa 160 za ziada kwa siku duniani.

Wasichana wawili kati ya watatu wanapika na kufanya usafi nyumbani, ambapo karibu nusu yao huchota maji na kuni.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, pia wanafanya kazi nyingi zaidi ambazo sio rahisi kuziona na hasa ni zile za nyumbani, kama kulea watoto na kuwaangalia wazee, ripoti hiyo imesema.

Imebainika kuwa, mzigo zaidi wa kazi kwa wasichana huongezeka kufuatana na muda: kati ya umri wa kati ya miaka 5 na 9, wasichana wanatumia asilimia 30 ya muda zaidi kufanya kazi, na wakifikisha umri wa miaka 14 muda huo huongezeka kwa asilimia 50.

Shughuli kama vile za kukusanya kuni na kuchota maji zinaweza kuwaweka wasichana kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, ripoti hiyo imesema.

Mfano nchini Somalia, wasichana wa kati ya umri wa miaka 10 na 14 hutumia saa 26 kwa wiki kufanya kazi za nyumbani, ikiwa ni muda zaidi kwenye nchi nyingine duniani. Burkina Faso na Yemen ni mataifa mengine yenye idadi kubwa ya kimatabaka kwenye ufanyaji kazi kati ya wavulana na wasichana.

“Wasichana wanajitoa muhanga kuahirisha kujifunza, kuku na badala yake wanafurahia utoto wao,” amesema Anju Malhotra kutoka Unicef.

Ripoti hii, ambayo imejumuisha takwimu za unyanyasaji, ndoa za utotoni, ukeketaji wa wanawake na elimu, imetolewa ikienda sambamba na siku ya mtoto wa kike duniani inayitarajiwa kuadhimishwa kidunia tarehe 11 ya mwezi October mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.