Pata taarifa kuu
SRI LANKA-SAUDI ARABIA

Serikali ya Sri Lanka yasema itabadili sheria kuhusu umri wa wasichana kwenda kufanya kazi za ndani nchini Saudi Arabia

Serikali ya Sri Lanka imesema kuwa itapitisha sheria rasmi kutoruhusu wasichana wa ndani toka nchini humo kwenda nchini Saudi Arabia kufanya kazi kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kunyongwa kwa raia wake. 

Waandamanaji wanawake nchini Sri Lanka wakiandamana hivi karibuni kupinga kunyongwa kwa mwenzao nchini Saudi Arabia
Waandamanaji wanawake nchini Sri Lanka wakiandamana hivi karibuni kupinga kunyongwa kwa mwenzao nchini Saudi Arabia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya nchi hiyo ilitoa tamko kali dhidi ya Serikali ya Saudi Arabia kufuatia kunyongwa kwa raia wake ambayo alipatikana na hatia ya kuhusika na mauji ya mtoto wa mwajiri wake aliyefia wakati akiwa kwenye uangalizi wake.

Serikali ya Sri Lanka imesema kuwa itabadili sheria ya umri wa wasichana hao kuruhusiwa kufanya kazi nchini Saudi Arabia na kufikia miaka 25 ambapo kiwango cha sasa cha kuruhusiwa kufanya kazi za ndani ni miaka 21.

Msemaji wa Serikali ya Sri Lanka Keheliya Rambukwella amethibitisha Serikali kuwa na mpango wa kubadili sheria hiyo na kuongeza kuwa jambo hilo haliwezi kufanywa kwa mara moja wala kwa usiku mmoja kwakua linahitaji muda pia.

Serikali ya nchi hiyo ilimuita nyumbani balozi wake nchini Saudi Arabia kufuatia kunyongwa kwa msichana Rizana Nafeek licha ya ombi la Serikali ya Sri Lanka na jumuiya ya kimataifa kutaka msichana huyo asinyongwe.

Zaidi ya robo tatu ya wasichana wa Sri Lanka wameajiriwa nchini Saudi Arabia kama wasichana wa ndani na hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Sri Lanka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.