Pata taarifa kuu
BOTSWANA

Botswana yamfukuza mchungaji wa Kimarekani anayetaka kuuawa kwa mashoga

Serikali ya Botswana imeagiza kufukuzwa nchini humo kwa mchungaji wa Kimarekani, Steven Andersonm saa chache baada ya mchungaji huyo kumaliza kipindi kwenye kituo kimoja cha redio ambapo alidai watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanapaswa kupigwa mawe hadi kufa.

Mchungaji Steven Anderson ambaye amefukuzwa nchini Botswana.
Mchungaji Steven Anderson ambaye amefukuzwa nchini Botswana. http://zackhunt.net
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Botswana, Ian Khama ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, yeye binafsi ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa kwa mchungaji huyo.

“Hatutaki kuona wala kusikia kauli za uchochezi kwenye nchi yetu. Hebu afanye hayo mambo akiwa kwenye taifa lake.” alisema Rais Khama.

Juma lililopitam Serikali ya Afrika Kusini ilimzuia mchungaji huyo kutembelea taifa hilo kutokana na kauli zake za ukosoaji mkubwa kuhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mapenzi ya jinsia nchini Botswana hayaruhusiwi kisheria, kama ilivyo pia kwa mataifa mengik ya bara la Afrika ambayo yamepiga marufuku.

Baada ya kuzuiliwa kutembelea nchi ya Afrika Kusini, baadae mchungaji huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Facebook kuwa “Tushukuru Mungu kwakuwa bado milango iko wazi Botswana.”

Mchungaji Anderson alikamatwa punde tu baada ya kumaliza mahojiano yake kwenye kituo cha redio cha GabzFM ambapo alikamatwa sambamba na mchungaji mwingine raia wa Botswana ambaye nae yuko mstari wa mbele kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

Mtangazaji wa kipindi hicho, alidai kuwa kwenye mahojiano yao, mchungaji Anderson alikuwa akisisitiza kuhusu kuuawa kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mchungaji Anderson mwenyewe amewaambia wanahabari kuwa, anaondoka nchini Botswana kwa hiari yake mwenyewe na sio kwamba amefukuzwa kama ilivyoripitia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.