Pata taarifa kuu
DRC-BENI-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea Beni baada ya makabiliano makali

Mamia ya waandamanaji waliandamana Jumatano hii Agosti 17 mjini Beni wakiwaomba viongozi tawala kukomesha mauaji ambayo yanaikumba wilaya hiyo kwa miaka miwili sasa na kujiuzulu kwa serikali. Lakini maandamano hayo yalikumbwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi, na kusababisha vifo vya watu wawili na zaidi ya ishirini kujeruhiwa.

Kwa uchache watu wawili waliuawa na ishirini kujeruhiwa katika maandamano dhidi ya serikali  Agosti 17, 2016, baada ya mauaji ya Beni, DRC.
Kwa uchache watu wawili waliuawa na ishirini kujeruhiwa katika maandamano dhidi ya serikali Agosti 17, 2016, baada ya mauaji ya Beni, DRC. ©RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya makabiliano hayo, hali ya utulivu imerejea, amesema mkuu wa wilaya hiyo.

Siku tatu baada ya mauaji yaliyoikumba wilaya ya Beni, raia wanaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu. Mamia ya raia waliingia mitaani Jumatano, wakipinga kile walichosema "serikali haiwajali kwa usalama wao". Baada ya makabiliano makali kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, "hali ya mji huo imedhibitiwa," Jean-Edmond Bwanakawa Nyonyi, alisema Jumatano jioni Agosti 17i. Mkuu wa wilaya ya Beni alichukua nafasi hiyo akiwataka raia kuwa "watulivu".

Kuhusu madai ya waandamanaji, Bw Bwanakawa Nyonyi amesema kuwa "kama kuna mtu ana maoni au madai, serikali iko tayari kumpokea." Meya pia amehakikisha kwamba "jeshi linafanya kile kilio chini ya uwezo wake kwa kuwalinda raia dhidi ya mauaji hayo."

Watu wawili wauawa

Jumatano wiki hii, maandamano alishuhudiwa katika miji miwili, Butembo na Oicha, lakini waandamanaji katika mji wa Beni, hawakuweza kujiunga na wenzao wa Oicha, baada ya kuzuiliwa nje kidogo ya mji.

Watu ambao inajulikana wamepoteza maisha mpaka sasa ni wawili, lakini idadi hii ni ya muda. Mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi aliuawa alifariki baada ya kurushiwa mawe, kwa mujibu wa Mkuu wa jiji. Inasemekana pia kuwa watu zaidi ya ishirini walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na wanne ambao walijeruhiwa kwa risasi na askari ambaye alijeruhiwa kwa kisu. Vijana kadhaa pia walikamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.