Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Rais Joseph Kabila wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda wakutana

Rais wa Jamhuri ya kidemokmarsaia y Congo Joseph Kabila amekutana na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame mjini Gisenyi mkowa wa Rubavu nchini Rwanda kujadili kuhusu masuala ya usalama wa eneo la mashariki mwa DRC.

Rais joseph Kabila wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda, mjini Gisenyi mkoa wa Rubavu nchini Rwanda Agosti 12 2016
Rais joseph Kabila wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda, mjini Gisenyi mkoa wa Rubavu nchini Rwanda Agosti 12 2016 CYRIL NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka kwenye Serikali ya Kinshasa, zinasema kuwa mazungumzo ya viongozi hao wawili, yamejikita katika kuimarisha usalama wa eneo la mashariki mwa DRC ambako makundi ya waasi wa kihutu kutoka Rwanda wa FDLR yameshutumiwa kuuzorotesha usalama wa eneo hilo.

Mwandishi wa RFI mjini Kigali anasema viongozi hao wamekutana mjini Gisenyi upande wa Rwanda jirani na mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Maafisa wa jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini wanasema katika kipindi cha wiki Kadhaa, jeshi limekuwa likikabiliana na waasi wa FDLR kutoka katika mikoa ya kivu kusini na kaskazini.

Eneo la mashariki mwa DRCongo limekuwa halina usalama likishuhudia harakati za makundi mbalimbali ya uasi, ambapo pamoja na kutangaza operesheni kadhaa zinazolenga kuwatimua waasi hao, ni vigumu kuthibitisha kuhusu mafanikio ya jeshi hilo.

Rais Joseph Kabila akimsalimia waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, mpakani baina ya nchi mbili za DRC na Rwanda, le 12 août 2016.
Rais Joseph Kabila akimsalimia waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, mpakani baina ya nchi mbili za DRC na Rwanda, le 12 août 2016. CYRIL NDEGEYA / AFP

Baadhi ya makundi hayo yamevivamia na kuvikalia vijiji vya eneo hilo na kusababisha wakaazi wa vijiji hivyo kubaki bila ya makaazi.

Mbali na usalama viongozi hao pia wanajadili suala la matumizi ya gesi ya methane inayozalisha umeme kutoka ziwa kivu na ambayo inatumiwa upande wa Rwanda
Mkutano huu unakuja siku chache baada ya rais Josephu Kabila, kukutana na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa uganda Agosti 04 kujaribu kuishawishi nchi hiyo, kuzidisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa ADF NALU wanaopigana mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.