Pata taarifa kuu
UFARANSA-LIBYA-USALAMA

Askari watatu wa Ufaransa wauawa katika "shughuli za serikali" Libya

Wizara ya Ulinzi imetangaza Jumatano hii vifo vya askari watatu wa Ufaransa, waliouawa wakiwa katika "shughuli za serikali" nchini Libya. "Tumepoteza askari wetu watatu[...] katika ajali ya helikopta," amesema François Hollande wakati alipokua akizuru kituo cha mafunzo ya Polisi katika eneo la Dordogne.

Vikosi vya Libya vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika mji wa Sirte, Libya, tarehe 12 Julai 2016.
Vikosi vya Libya vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika mji wa Sirte, Libya, tarehe 12 Julai 2016. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapema leo asubuhi, msemaji wa serikali ya Ufaransa, Stéphane Le Foll, amethibitisha kuwepo kwa vikosi maalum vya Uifaransa nchini Libya kwa kupambana dhidi ya wanajihadi.

Askari watatu wa Ufaransa wameuawa nchini Libya katika "ajali ya helikopta" wakatiambapo walikua katika shughuli ya kikazi ya upelelezi, amesema mapema mchana Francois Hollande wakati alipokua akizuru kituo cha mafunzo cha polisi katika eneo la Dordogne.

Lakini katika siku za hivi karibuni, taarifa zilizochapishwa kwenye magazeti zilibaini vifo vya raia wawili kutoka nchi za kimagharibi, askari wawili wa vikosi maalum vya Ufaransa, waliouawa katika ajali ya helikopta ya Libya aina ya Mi-35 waliokuwemo, iliyokua ikitumiwa na majeshi ya jenerali Haftar. Helikopta iliyodunguliwa Jumapili Julai 17 kwa kombora katika anga ya kijiji cha al-Makroun, kilomita 70 kutoka mji wa Benghazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.