Pata taarifa kuu
LIBYA-IS

Libya: askari 34 wauawa katika mapigano na IS

Askari wasiopungua 34 wa vikosi vya Serikali waliuawa Jumanne wiki hii katika mapigano makali na wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic State (IS) wanaozingira kwa miezi kadhaa eneo la katikati la ngome yao ya Sirte, kwa mujibu wa chanzo cha matabibu.

Vikosi vya serikali ya umoja vikijaribu kuingia katika mji wa Sirte.
Vikosi vya serikali ya umoja vikijaribu kuingia katika mji wa Sirte. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne ilikua siku mbaya kwa majeshi ya Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) tangu Mei 12 yalipoanza mashambulizi yao kwa lengo la kuudhibiti mji wa Sirte (kaskazini) unaodhibitiwa na wanajihadi.

Hayo yakijiri watu 29 waliuawa na na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa ghala la silaha katika mji wa mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli kufuatia makabiliano kati ya raia wanaobebelea silaha na wanamgambo, kwa mujibu wa maafisa.

Jumanne katika mji wa Sirte, kilomita 450 mashariki mwa mji mkuu Tripoli, mapigano makali baina ya vikosi vya Serikali ya umoja (GNA) vinavyotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na wanajihadi katika mji huo wanaodhibiti tangu Juni 2015, kulingana na uongozi wa kijeshi.

"Jeshi letu linasonga mbele kutoka pande zote dhidi ya ngome ya wanajihadi, likisaidiwa na vifaru na jeshi la anga," uongozi wa jeshi umeongeza.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na chanzo cha matabibu katika mji wa Misrata, "watu 34 wameuawa na 100 waliojeruhiwa" miongoni mwa vikosi vya vinavyounga mkono serikali katika mji wa Sirte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.