Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-VURUGU

Cote d'Ivoire: makabiliano kati ya wanafunzi na polisi

Nchini Cote d'Ivoire, Jumatatu hii Julai 18 kulitokea makubaliano makali kati ya baadhi ya wanafunzi wa polisi, katika Chuo Kikuu cha Cocody, katikati mwa mji wa Abidjan. Wanafunzi wamekua wakipinga hasa dhidi ya mazingira ya visomo.

Mabweni mapya ya Houphouët-Boigny  (Chuo Kikuu cha zamani cha Cocody).
Mabweni mapya ya Houphouët-Boigny (Chuo Kikuu cha zamani cha Cocody). RFI/Cécile Lavolot
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu alaasiri, mawe yalikua bado yakijazana katika chuo hicho. Mawe hayo ndio yalitumiwa katika makabiliano hayo. Madirisha ya baadhi ya madarasa yalivunjwa na magari yalichomwa moto. Hata hivyo hivyo, hali ya utulivu imerejea, lakini askari polisi wengi walikuwa wengi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wao, aliyeongea na RFI, vikosi vya usalama ilibidi waingilia kati wakati ambapo chama cha wanafunzi (FESCI), ulio karibu na upinzani na kuchukuliwa kama chenye kuchochea vurugu na wapinzani wake, kilikua kikizuia wanafunzi kuingia madarasani.

"Wakati kunatokea hvurugu zenye lengo la kuhatarisha usalama wa raia, ni lazima kuingilia kati," chanzo cha polisi kimesema.

Madai haya yanatupiliwa mbali na wajumbe wa chama cha wanafunzi (FESCI), ambao wanahakikisha kwamba wao walikua walikua wamegoma. Kwa mujibu wa chama hicho, wanafunzi zaidi ya 50 walikamatwa na wengine kadhaa walijeruhiwa. askari watatu pia walijeruhiwa, kulingana na Wizara ya Mambo ya ndani.

Imekuwa ni wiki moja sasa tangu cham cha wanafunzi (FESCI) kuwataka wanafunzi wafanye mgomo wakipinga dhidi ya mazingira yao ya visomo. Shahada ya juu ni ghali mno au pia mitihani ni ya kipekee, hasira kwa wanafunzi ni kubwa na mvutano umekua ukitokea mara kwa mara ndani ya chuo kikuu cha mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.