Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Shambulio jipya Beni: watu zaidi ya 9 wauawa

Watu wasiopungua tisa wakiwemo wanawake watano wameuawa Jumanne hii Julai 5 na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Uganda wa ADF katika vijiji vya Tenambo, Nzanza na Mamiki, katika mji wa Oicha, kilomita 30 kutoka mji wa Beni (Kivu Kaskazini).

Wanajeshi wa Monusco wakiwa kwenye doria mjini Beni
Wanajeshi wa Monusco wakiwa kwenye doria mjini Beni UN Photo/Sylvain Liechti
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa wilaya ya Beni, Kalonda Amisi amesema idadi hii inaweza ikaongezeka.

Bw Amisi amesema kundi hilo la wahalifu walitekeleza kitendo hiki kiovu katika muda wa saa 10:00 Alfajiri hadi 12:00 asubuhi wakati mvua kubwa zilipokua zikinyesha. Baadhi ya wahalifu hao walikua wakiiba mifugo na mali wakati ambapo wengine walikua wakiua watu kwa mapanga au kwa risasi, ameseam Mkuu wa wilaya ya Beni.

Zoezi la utafutajilinaendelea ili kupata iwezekanavyo waathirika wengine, anasema, Kalonda Amisi.

Ni katika eneo hili ambapo kwa karibu miaka miwili, mauaji yamekua yakishuhudiwa mara kwa mara. Jeshi la Congo (FARDC) na askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) wanalihusisha kundi la waasi wa Uganda ADF katika visa hivi vya mauaji, ingawa madai haya yanatupiliwa mbali na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Tenambo.

Vyama vya kiraia vya wilayani Beni wilaya, kwa upande wao wanawalauamu askari wa Congo kama wale wa Umoja wa Mataifa ambao hawakuingilia kati kwa kuokoa maisha ya raia hao wakati ambapo wanapiga kambi karibu mitaa kadhaa na eneo la tukio.

Wanajeshi wa Serikali wakiwa kwenye doria mjini Beni mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wa Serikali wakiwa kwenye doria mjini Beni mashariki mwa DRC. UN Photo/Sylvain Liechti

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.