Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIMONE GBAGBO

ICC bado yamtaka Simone Gbagbo kujibu tuhuma

Wakati mahakama nchini Cote d’Ivoire ikisikiliza jana kesi ya Simone Bagbo, mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo rais Laurent Gbagbo, anaetuhumiwa makosa ya uhalifu wa kivita, mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC inasema bado inamuhitaji Simone Gbagbo kujibu tuhuma dhidi yake mbele ya mahakama hiyo ya ICC.

Simone Gbagbo Mke wa rais wa zamani wa Cote d’Ivoire Laurent Gbagbo
Simone Gbagbo Mke wa rais wa zamani wa Cote d’Ivoire Laurent Gbagbo REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Mke huyo wa rais wa zamani wa Cote d’Ivoire awali alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika uvunjifu wa Usalama wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 -2011.

Upande wa Utetezi kupitia wakili Rodrigue Dadjee unakosoa namna kesi hiyo inavyoendeshwa na kuona kwamba inaendeshwa kisiasa zaidi na lengo ni kumuhukumu tu Simone Gbagbo.

Upande wake msemaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC
Oriene Maillet anasema hati ya kukamatwa kwa Simone Gbagbo bado ipo, serikali ya Cote d’ivoire inalazimika kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.