Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Nigeria yawapokea wapiganaji 800 wa Boko Haram

Nigeria imewapokea wapiganaji 800 wa kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram baada ya wapiganaji hawa kutangaza kuwa wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.

Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015.
Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015. AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao kwa sasa wamewekwa katika kituo maalum wakiendelea kupata mafunzo ya msimamo wastani wa kidini.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanania ya kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaokiri na kutubu makosa yao.

Hivi karibuni serikali ya Nigeria imetangaza kiuwepo na mpango mahsusi wa “Operation Safe Corridor” unaolenga kuwapokea wapiganaji wa kundi la Boko Haram watakaojisalimisha

Kundi la Boko Haram limewaua maelfu ya raia wa Nigeria tangu lianzishe harakati zake katika nchi hiyo na nchi jirani.

Serikali imetangaza kwamba wapiganaji hao waliojisalimisha wanatazamiwa kufunzwa jinsi gani ya kujitafutia riziki kabla ya kupewa mtaji wa kuanza upya maisha yao.

Kwa sasa serikali itakua na kazi kubwa ya kuwahamasisha raia, hasa wale ambao ndugu au jamaa zao waliuawa na kundi hili, kuishi pamoja nao.

Inaaminika kuwa zaidi ya watu 10,000 waliuawa na milioni moja waliyayahama makazi yao tangu kundi hili lianzishe harakati zake nchini humo miaka 7 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.