Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAENDELEO

Rais Magufuli awataka wakuu wa mikoa kuwajibika

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewata wakuu wa mikoa kufanya kazi bila uoga katika kutekeleza majukumu yao na kutekeleza ahadi zilizoahidiwa katika ilani ya Uchaguzi uliopita na kusimamia shughuli za serikali kwa kufuata utawala wa sheria.

John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015.
John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Rais Dk. John Pombe Magufuli ametoa wito huo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa hao ikulu jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa viongozi wanapswa kufanya kazi kwa uadilifu ili kuwasaidia raia masikini kuondokana na matatizo yao.

Rais John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hususan mikoa iliyoko mipakani na nchi jirani kuhakikisha wanasimamia hali ya usalama ili kuepusha raia kuishi kwa wasiwasi wanapotekeleza majukumu yao.

Rais Magufuli ameoonyesha kukerwa na tabia ya watu hususan vijana kutofanya kazi na kujielekeza katika shughuli ambazo hazina tija na kwamba wakuu wa mikoa wanawajibika kushughulikia tatizo hilo na ikibidi vijana walazimishwe kufanya kazi.

Dk. Magufuli anaona kuwa Uozo katika Halmashauri likiwemo tatizo la wafanyakazi hewa inaonekana kuwa miongoni changamoto watakazokumbana nazo na kuwajibika kuzishughulikia ili kudhibiti fedha za umma.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha mikoa yao haina njaa kwa kuwa uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha upo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.