Pata taarifa kuu
EU-DRC-UHURU WA RAIA

EU yaitolea wito serikali ya DRC kuheshimu uhuru wa raia

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, ukiungwa mkono na balozi za umoja huo nchini, umetolea wito serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu majukumu yake ya kitaifa, hususan Katiba, na ahadi za kimataifa, ikimaanishwa Mikataba ya Cotonou

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Oktoba mwaka jana katika mji wa Beni.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Oktoba mwaka jana katika mji wa Beni. © AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya unasema kutiwa wasiwasi na kuongezeka kwa vitendo vya vitisho na unyanyasaji.

Katika utangulizi wake, Umoja wa Ulaya unakumbusha kwamba "katika kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi, kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa raia ni mambo muhimu ili kuwezesha uchaguzi ulio uwazi, halali na wenye kuaminika. "

Wakati ambapo Rais Joseph Kabila aliitisha mjadala wa kitaifa tangu mwishoni mwa mwezi Novemba, mazungumzo ambayo yamechelewa kufanyika, Umoja wa Ulaya unasisitiza : "wito kwa mazungumzo ya kisiasa unapaswa kwenda sambamba na haki ya kila mtu ya kujieleza kwa uhuru." Mambo mengi yanaonekana kuusumbua Umoja wa Ulaya. Na kwanza kabisa, "ripoti inayohusu ongezeko la vitendo vya unyanyasaji na vitisho vinavyowalenga viongozi wa kisiasa, wajumbe wa vyama vya kiraia na vyombo vya habari."

Sababu ya pili ya wasiwasi, ni pamoja na vikwazo vinavyoukabili Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo (MONUSCO) kwa kile kinachoendana na "kuangalia na kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu". Katika tamko hili, Umoja wa Ulaya unasisitiza kutokana na kwamba, MONUSCO, ambayo Ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inategemea, na kufanya shughuli zake kulingana na azimio 2211 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Azimio ambalo linasema kwamba majukumu yake pia ni "kuangalia na kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na makosa au uhalifu unaotokea katika uchaguzi. "

Hata hivyo, Umoja wa Ulaya unasema utaendelea kusaidia mageuzi ya vyombo vya sheria kupitia mpango wake, utakaogharimu Euro milioni 40 kutoka Mfuko wa Ulaya kwa Maendeleo, kwa minajili ya "kuhakikisha kwamba raia wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanapata haki sawa bila upendeleo kwa vyombo vya sheria [...] kulingana na sheria pamoja na Katiba ya nchi hiyo. "

Itakumbuka kwamba, balozi kadhaa za nchi za Magharibi zilielezea wasiwasi wao baada ya uamuzi dhidi ya wanaharakati sita wa chama cha kiraia cha LUCHA, walioadhibiwa kifungo cha miaka miwili jela katika mahakama ya mwanzo, na kisha miezi sita baada ya kukata rufaa.

Serikali ya Congo ililaani taarifa hizo za jumuiya ya kimataifa, ikishtumu kwamba ni mwenendo mpya wa ukoloni na kusisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya sheria vya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.