Pata taarifa kuu
DRC-UN-UE-AU-OIF-SIASA

DRC: UN, AU, EU na OIF vyaomba uchaguzi kufanyika "kwa wakati mzuri"

Taasisi nne za kimataifa zimetoa tangazo la pamoja zikiomba uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ufanyike kwa wakati mzuri. Tangazo hilo halikuweka wazi kuhusu kuheshimu Katiba na mihula inayopangwa na Katiba.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Taaaasisi hizo ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya kimataifa ya nchini zinazozungumza Kifaransa (OIF).

Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unapaswa kufanyika "kwa wakati mzuri", tangazo hilo limebaini. Taasisi hii zinaunga mkono kufanyika kwa mazungumzo ya kisiasa kwa lengo la maandalizi ya uchaguzi na zinaunga mkono kazi ya msuluhisi Edem Kodjo.

Taasisi hizi nne zinasisitiza umuhimu wa uchaguzi huu, ambao unapaswa kufanyika ndani ya miezi tisa. Tangazo hili linasema umuhimu wa kufanyika uchaguzi huu "kwa wakati mzuri" na imesisitiza kuhusu uheshimishwaji wa mfumo wa Katiba.

Hakuna onyo, hata hivyo, juu ya kufanyiwa vitisho na kukamatwa kwa baadhi ya wanasiasa na ukiukaji wa haki za binadamu wakati waangalizi wanaamini kwamba tayari hali hiyo inatishia uaminifu wa mchakato wa uchaguzi.

Taasisi hizi nne pia zimetoa wito kwa wadau wote wa kisiasa nchini Congo kutoa "ushirikiano wao kamili" kwa Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo. Ujumbe kwa wale walio katika upinzani, ambao hawakutaka kukutana naye, kama muungano wa upinzani au G7. Ujumbe pia kwa mpinzani Etienne Tshisekedi na chama chake cha UDPS ambapo baada ya kukutana na Edem Kodjo walikataa mazungumzo kama jinsi yalivyoitishwa na Joseph Kabila.

Ili kuwahakikishia wadau wote, taasisi hizi nne zimeelezea Mkataba wa Afrika juu ya Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, ambavyo vinaeleza katika ibara ya 5 uheshimishwaji wa utaratibu wa kikatiba na kupishana madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.