Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-MWANAHABARI

Somalia: mwanahabari aliojihusisha na ugaidi ahukumiwa adhabu ya kifo

Mwandishi wa habari wa Somalia, Hassan Hanafi Haji, aliejiunga na wapiganaji wa kundi la Kiislam la Al Shabab, amehukumiwa adhabu ya kifo Alhamisi hii Machi 3 mjini Mogadishu kwa kosa la kupanga mauaji ya wafanyakazi wenzake 5 kati ya mwaka 2007 na 2010.

Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab
Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Hassan Hanafi amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya mahakama kumkuta na hatia ya mashtaka yote dhidi yake," amesema jaji Hassan Ali. "Vielelezo vya ushahidi na mashahidi vinaonyesha kuwa alihusika katika kwa kiwango kikubwa katika mpango na utekelezaji wa mauaji ya waandishi wa habari, ameongeza Hassan Ali".  Somalia ni nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa mahakama, Hassan Hanafi Haji alitambua makosa yake pamoja na kuwa katika kundi la Al Shabab. Bado anaweza kukata rufaa. Nchini Somalia, kawaida, watu wanaohukumiwa adhabu ya kifo, hupigwa risasi.

Hassan Hanafi Haji alikamatwa Agosti 2014 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na alisafirishwa nchini Somalia mwishoni mwa mwaka huo. Alhamisi hii, waandishi wa habari kadhaa wamehudhuria kesi hiyo mjini Mogadishu.

Somalia ni moja ya nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari: waandishi wa habari 33 kutoka Somalia wameuawa nchini humo tangu mwaka 2007 ya kundi la Al Shabab kuzidisha mashambulizi yake katika maeneo mablimbali nchi Somalia, kwa mujibu wa Shirika la Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ).

Kundi la Al Shabab, lenye uhusiano na al-Qaida, wameapa kuivunja serikali dhaifu ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na kusaidiwa na kikosi imara cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) chenye wanajeshi 22,000. Wapiganaji wa Al Shabab, hivi karibuni, waliendesha mashambulizi makubwa dhidi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) na kutekeleza mashambulizi yaliosababisha vifo vingi vya watu dhidi hoteli na migahawa mjini Mogadishu. Wamekua wakirusha ujumbe wao na itikadi zao kupitia radio yao na video za propaganda ambazo wamekua wakirusha kwenye mtandao wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.