Pata taarifa kuu
UINGEREZA-URUSI-USALAMA WA ANGA

London yaonya kuhusu ukosefu wa usalama katika viwanja vya ndege

Kipaumbele ni kuimarisha udhibiti katika maeneo ambayo Daesh inaonekana "imara" kwa mujibu wa London ...

Uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh, Misri, Novemba 7, 2015.
Uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh, Misri, Novemba 7, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi imetanda, siku nane baada ya ajali ya ndege ya Urusi nchini Misri iliyosababishwa na shambulizi, kwa mujibu wa London, Washington na wataalam karibu wote. Wito umekua ukitolewa kwa kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, usalam ambao unapaswa kuwa kwa "kiwango cha juu" na "kufanyiwa mapitio kila mara" katika majengo ya viwanja vya ndege ", waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond amesema.

Kipaumbele ni kuimarisha udhibiti katika maeneo ambayo Daesh inaonekana imara, ambayo ilihusika kwa mashambulizi ya ndege ya shirika la Urusi yaliyosababisha watu 224 waliokua katika ndege hiyo kupoteza maisha”, kwa mujibu wa London.

Uingereza ina wasiwasi na athari za ajali, kwa sababu uamuzi wa London kufuta safari za ndegeza kawaida umewaacha watalii 20,000 wa Uingereza katika mji wa mapimziko wa Sharm el-Sheikh. Philip Hammond amesema kuwa watalii "3300"miongoni mwao wamerejeanchini Uingereza na kwa jumla "5000" watakuwa wamewasili Jumapili usiku.

Uingereza na Marekani ni nchi za kwanza zilizodai kuwa kuna uwezekano kuwa ndege ya Urusi ilishambuliwa kwa bomu. Baada ya kuwa na mashaka, Urusi sasa inaonekana kukybali madai ya nchi hizi mbili, bila hata hivyo kusema rasmi, baada ya kusimamisha safari zote za ndege za abiri kwenda Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.