Pata taarifa kuu
MAREKANI-CAMEROON-USHIRIKIANO-USALAMA

Marekani: Barack Obama atuma askari 300 Cameroon

Marekani iitapeleka askari 300 nchini Cameroon kwa mwaliko wa serikali ya Yaounde. Tangazo hili limeyotolewa na Ikulu ya Marekani na Baraza la wawakilishi limefahamishwa.

Rais wa Marekani Barack Obama akisisitiza kupelekwa Cameroon kwa askari 300 wa Marekani ili kupambana na Boko Haram.
Rais wa Marekani Barack Obama akisisitiza kupelekwa Cameroon kwa askari 300 wa Marekani ili kupambana na Boko Haram. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupelekwa kwa askari wa Marekani nchini Cameroon ni sehemu ya mapambano dhidi ya kundi la Islamic State Afrika Magharibi (kundi la zamani la Boko Haram).

Askari 90 wako nchini Cameroon tangu mwanzoni mwa wiki hii, na idadi ya askari hao itafikia hadi 300 wiki ijayo, ikiwa ni pamoja na wataalam katika masuala ya ujasusi.

Cameroon ni sehemu ya muungano dhidi ya kundi la waasi wa kundi la Islamic State Afrika Magharibi (zamani Boko Haram) ambalo linaendesha kwa miezi kadhaa mashambulizi na umwagaji damu kaskazini mashariki mwa Nigeria, ngome yao kuu ya kihistoriaili kuendesha mashambulizi katika nchi jirani za bonde la Ziwa Chad: Chad, Cameroon na Niger.

Tangu Jumatatu, askari 90 wa Marekani waliwasili nchini Cameroon na kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, idadi yao itafikia 300. " Wanajeshi wa Marekani ambao tumeanza kupeleka nchini Cameroon, ni kwa mwaliko wa serikali ya Cameroon, na watafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ", amesema Josh Earnest, msemaji wa Barack Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.