Pata taarifa kuu
BURUNDI-SHAMBULIO-USALAMA

Burundi: mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi auawa

Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana, mkuu wa zamani wa majeshi kutoka kundi la zamani la waasi la Cndd-Fdd na mmoja wa wababe wa utawala wa Pierre Nkurunziza ameuawa Jumapili asubuhi Agosti 2 mjini Bujumbura katika shambulio la roketi.

Wanajeshi wa Burundi katika mitaa ya mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, Mei 2015.
Wanajeshi wa Burundi katika mitaa ya mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, Mei 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wakati hu huo, mwandishi wa Idhaa ya Kifaransa ya RFI mjini Bujumbura, Esdras Ndikumana amekamatwa na afisaa wa Idara ya Ujasusi wakati alipokua akiendesha kazi yake ya kutafuta habari katika eneo la tukio. Esdras Ndikumana amepigwa vikali katika ofisi za Idara ya Ujasusi kabla ya kuachiliwa huru.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amelihutubia taifa Jumapili jioni, ambapo amelaani shambulio hilo, huku aliwatola wito raia kuwa watulivu. Msemaji wa rais Pierre Nkurunziza, Gervais Abayeho, amebaini kwamba rais wa Burundi "ametoa muda wa siku saba ili uchunguzi unaoendelea uwe umekamilika na wahusika wa mauaji hayo waweze kujulikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ".

Kwa mujibu wa mashahidi, gari la luteni jenerali Adolphe Nshimirimana lililengwa kwa mashambulizi ya roketi mbili, kisha kufyatuliwa risasi nyingi asubuhi ya Jumapili mwishoni mwa juma hili. Tukio hilo limetokea karibu na hospitali ya Mfalme Khaled katika mji mkuu, Bujumbura. Vikosi vya usalama vimearifu kuwa vimewakamata watu saba wanaoshukiwa kuendesha shambulio hilo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Muda mfupi kabla ya saa sita mchana, mshauri mkuu wa rais anaye husika na maswala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe, amethibitisha kifo cha afisa huyo mwandamizi katika jesi. " Nimempoteza ndugu, jamaa. Ninasikitika kwa kweli na kifo cha Adolphe Nshimirimana, ambaye hayupo tena katika ulimwengu huu ", Willy Nyamitwe ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mkuu wa zamani wa majeshi kutoka kundi la zamani la waasi la Cndd-Fdd na mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa mwezi Novemba mwaka 2014 na jenerali mwenye msimamo wa wastani Godefroid Niyombare.

Adolphe Nshimirimana alikua mmoja wa wababe wa utawala wa Pierre Nkurunziza, ambaye alionekana kuwa karibu na rais huyo kwa kipindi kirefu cha utawala wake. Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana alikua aliteuliwa afisaa anayehusika na safari za rais, lakini, kwa ukweli, aliendelea kujishughulisha na uongozi wa jeshi na kazi zingine za kumlindia usalama rais Pierre Nkurunziza, huku akiwa na ushawishi mkubwa katika chama tawala cha Cndd-Fdd.

Luteni jenerali Nshimirimana alionekana kama mwaandaaji na mpangiliaji wa ukandamizaji ulioshuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni, na pia alikua mmoja wa maafisa wa jeshi waliozima jaribio la mapinduzi lililotokea mwishoni mwa mwezi Mei.

Kifo cha jenerali adolphe Nshimirimana kinakuja wiki moja baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais, ushindi unaompelekea rais huyo kuanza awamu ya tatu, ambayo imezua utata nchini Burundi.

Mwandishi wa RFI akamatwa na kupigwa

Muda mfupi baada ya shambulio hilo, mwandishi wetu nchini Burundi, Esdras Ndikumana, alijielekeza katika eneo la shambulio, na wakati alipokuwa akipiga picha, alikamatwa na kupelekwa kwenye makao makuu ya Idara ya Ujasusi. Huko, alipigwa na kuitwa " mwandishi wa habari adui ". Baadae aliachiliwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu ya kidole chake kilichovunjwa.

RFI inatolea wito Ofisi ya rais wa Burundi kupinga kitendo hicho cha ukatili alichofanyiwa mwandishi wetu.

Adolphe Nshimirimana, alikua miongoni mwa wanaomuunga mkono Pierre Nkurunziza

Adolphe Nshimirimana alikuwa mwaminifu kati ya waaminifu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, mkono wake wa kulia, mtu muhimu kwa usalama wake. Alikuwa mmoja wa wale ambao rais alijua angeweza kutegemea. Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana kama rais Pierre Nkurunziza, walifanya vita vya maguguni kutoka kundi la waasi wa kihutu la Cndd-Fdd, ambacho kwa sasa ni chama tawala. Luteni jenerali Nshimirimana aliwahi kuwa mkuu wa majeshi ya Burundi katika miaka ya 2005 hadi 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.