Pata taarifa kuu
KENYA-AL SHABAB-UGAIDI-USALAMA

Kenya: raia waomboleza vifo vya watu 14

Wakenya wanaendelea kuomboleza vifo vya watu 14, wengi wao wakiwa wachimba midogi waliouawa katika Kaunti ya Mandera baada ya kushambuliwa na kundi la Al Shabab kutoka Somalia, usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii.

Wanajeshi wa Kenya, mjini Nairobi, wakielekea katika jengo la Westgate, lililoshambuliwa na kundi linaloshukiwa kuwa la Al Shabab miaka ya hivi karibuni.
Wanajeshi wa Kenya, mjini Nairobi, wakielekea katika jengo la Westgate, lililoshambuliwa na kundi linaloshukiwa kuwa la Al Shabab miaka ya hivi karibuni. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Watu 14 waliuawa na zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya washukiwa wa kundi la Al Shabab kuvamia kijiji cha Soko Mbuzi Karibu na mji wa Mandera, nchini Kenya.

Shambulio hili lilithibitishwa na Kamishena wa Kaunti ya Mandera Alex Ole Nkoyo ambaye alisema wanamgambo hao walivamia kijiji hicho saa saba usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii.

Kundi la Al Shabab limeendelea kutekeza uharibifu mkubwa na mauaji katika maeneo mbalimbali nchini Kenya, hasa katika maeneo yaliyo karibu na mpaka na Somalia.

Makabiliano makali kati ya vyombo vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab yalitokea Jumatatu usiku Mei 25, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Kijiji cha Yumbis na maeneo mengine yaliyopembezoni katika Kaunti ya Garissa, yalilengwa na wanamgambo hao wa Al Shabab.

Kenya imekua ikilengwa na mashambulizi ya Al Shabab, baada tu nchi hiyo kuchukua uamzi wa kuwatuma wanajeshi wake kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika kusimamia amnai nchini Somalia.

Hata hivyo serikali ya Kenya imeapa kutowaondoa wanajeshi wake nchini Somalia, licha ya vitisho na mashambulio hayo yanayotekelezwa na Al Shabab nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.