Pata taarifa kuu
HRW-KENYA-TUHUMA-USALAMA-HAKI

HRW: vikosi vya usalama vya Kenya vilitekeleza mauaji

Mwaka mmoja sasa, tangu wanamgambo wa Al Shabab kuendesha mfululizo wa mashambuliziyaliyogharimu maisha ya watu wengi katika pwani ya Kenya, katika kaunti ya Lamu na Tana River.

Vikosi vya usalama vya Kenya sio tu kushindwa kulindia usalama wakazi dhidi Al Shabab, lakini pia kuhusika katika mauaji ya raia wakati wa operesheni zao.
Vikosi vya usalama vya Kenya sio tu kushindwa kulindia usalama wakazi dhidi Al Shabab, lakini pia kuhusika katika mauaji ya raia wakati wa operesheni zao. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha wiki hizo tano mwezi Juni na Julai, abiria waliokua katika basi walilengwa na mashambilizi hayo bila kusahau vijiji angalau vinane viliyoshambuliwa na kundi hili la wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia. Watu 87, ikiwa ni pamoja na askari polisi wanne waliuawa.

Lakini idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi ya Al Shabab iliendelea kuongezeka kufuatia kuongezwka kwa mashambulizi ya kundi hili. hata hivyo Jeshi na polisi kwa upande wao walijihusisha wakati huo na mauaji ya raia wa kawaida.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Human Right Watch pamoja na Tume ya haki za binadamu nchini Kinya, katika ripoti viliyotoa Jumatatu wiki hii vimelani mauaji hayo

Ripoti hiyo inavinyooshea vidole vikosi vya usalama vya Kenya kiuwa vilihusika na mauaji dhidi ya waislamu na raia kutoka Somalia. Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha jinsi gani vikosi vya usalama vya Kenya vilihindwa kulinda wakazi wa Kaunti hizo dhidi ya mashambulizi ya Al Shabab kutokana na ukosefu wa vifaa na ukosefu pia wa uratibu. Jeshi na Polisi walikua wakiwasili wakichelewa katika maeneo ya matukio au wasijielekezi hata katika maeneo kulikotokea mashambulizi ya Al Shabab, licha ya kupata taarifa kuhusu mashambulizi hayo.

" Wakati wa opereshi za jeshi au polisi, badala ya kufanya kazi na jamii ili kuelewa jinsi gani mashambulizi yalivyotokea na kutambua wale ambao walihusika, vikosi vya usalama vilikua vikiwalenga Waislamu na watu kutoka jamii ya Wasomalia ", amesema Maria Burnett, mtafiti katika Human Rights Watch.

" Watu wa jumuiya hizo ndio waliokuwa wakikamatwa kwa idadi kubwa, wakipigwa na kuwekwa kizuizini, ameendelea kusema Burnett. Mbinu za kibaguzi ziliyotolewa katika operesheni hizo zilitufanya sisi kuwa na wasiwasi sisa ", amesikitika mtafiti huyo katika Human Right watch.

Jeshi au polisi ya Kenya havijaeleza chochote kuhusu tuhuma hizo dhidi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.