Pata taarifa kuu
DRC-MADASCAR-CAF-SOKA-AFCON 2017

AFCON 2017 : DRC yaiburuza Madagascar

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepata ushimdi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar. Timu hizi mbili ambazo ni miongoni mwa kundi B katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la mataifa barani Afrika 2017 zimechuana Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Mchezaji wa DR Congo Yannick Bolasie.
Mchezaji wa DR Congo Yannick Bolasie. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

DR Congo ilikua na matumaini makubwa ya kupata ushindi mnono Jumapili Juni 14 mwaka 2015 mjini Kinshasa. Lakini timu hiyo ya taifa ya Congo imepata ushindi huo licha ya kuwa timu ya taifa ya Madagascar kuonyesha mchezo mzuri ikiwa ugenini mjini Kinshasa. Hata hivyo DR Congo imeandikisha alama tatu bao ya kuiadhibu Madagascar kwa mabao 2-1. Kundi B linaundwa na DR Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Angola.

Bao la kwanza la DR Congo limewekwa kimyani na Firmin Mubele, baada ya kupewa pasi na Yannick Bolasie katika dakika ya (58).

Katika dakika ya (73), mlinzi Leopards, Joel Kimwaki alichezesha nyavu za Madagascar na kuipatishia timu yake bao la pili kwa pasi aliyoipata kupitia Firmin Mubele, ambaye ameonekana kuwa mchezaji bora asiyejipendelea kufunga mwenyewe, bali kushirikiana na wengine kwa kuipatishia timu yake ushindi.

Wachezaji wa Florent Ibengé wamewatoa kijasho baridi wafuasi wao, baada ya kufungwa bao la mchezaji wa Madagascar na hivyo kupunguza idadi ya mabao katika dakika ya 76 ya mchezo. Jeannot Vombola alijikuta mpira ukichezea nyavuni katika lango lake. Goli hilo la Madagascar lilipelekea timu hiyo kuja juu ili kuweza kutoka sare ya mabao mawili na DR Congo bila mafanikio.

Hadi dakika tisini za mchezo, timu ya DR Congo ilijikuta imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar. hadi kipenga cha mwisho mashabiki wa DR Congo walijikuta wamevamia uwanja bila kujua kutoka na furaha ya ushindi wa timu yao.(76).

DR Congo kwa sasa inachukua nafasi ya pili katika kundi B kabla ya kwenda kucheza dhidi ya Afrika ya Kati, tarehe 4, 5 au 6 Septemba, wakati wa siku ya pili ya michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.

Wakati huo huo Niger imeifunga Namibia bao 1-0 katika mechi ya kufuza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017, huku togo yikiibwagiza Liberia (2-1) cameroon kwa upande imeifunga kwa tabu sana Mauritania bao 1-0. Afrika Kusini imetoka sare na Gambia ya kutofungana. Tanzania imeangukia pua kwa kuburuzwa na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.