Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-SIASA-MAZUNGUMZO

Libya: wadau wakutana kwa matumaini ya kuundwa serikali ya umoja

Pande husika katika mgogoro unaondelea nchini Libya zinakutana upya kwa mazungumzo kwa mara ya nne nchini Morocco, katika mji wa Skhirat kwa lengo la kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Bernardino Leon, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, katika mkutano uliopita nchini Morocco kuhusu Libya, Machi 5 mwaka 2015.
Bernardino Leon, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, katika mkutano uliopita nchini Morocco kuhusu Libya, Machi 5 mwaka 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanalenga kuunda serikali ya umoja katika hali ya kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Libya kwa sasa ina serikali mbili na baraza mbili za bunge. Serikali moja na bunge ambavyo havitambuliwi kimataifa vinaendesha shughuli zao katika mji wa Tripoli, na serikali nyingine na bunge vinavoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa vinaendesha harakati zao katika mji wa Tobrouk, mashariki mwa nchi

Kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya, hatua muhimu huenda ikapatikana katika mazungumzo hayo mapya. Mwakilishi wa Ujumbe huo, Bernardino Leon, amesema ana matumaini kuwa huenda serikali ya umoja ikaundwa kupitia mazungumzo hayo.

Mikutano kadhaa ilifanyika katika mji wa Skhirat tangu mwezi Januari uliyopita ili kujaribu kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Libya. Baada ya kufanikiwa kusitisha mapigano, baraza mbili tofauti za bunge ziliamua baadae kujadili suala la kuumdwa kwa taasisi mpya za uongozi wa nchi. Mazungumzo hayo yaliendelea kati ya mwezi Machi na Aprili katika mji wa Skhirat.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.