Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENYA-DIPLOMASIA-AL SHABAB-USALAMA

John Kerry ziarani Kenya

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry yuko nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu tangu Jumamosi Mei 3 hadi Mei 5.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jom Kenyatta, Nairobi, Mei 3 mwaka 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jom Kenyatta, Nairobi, Mei 3 mwaka 2015. AFP PHOTO/TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Usalama, mapambano dhidi ya wanaqmgambo wa Al Shabab kutoka Somalia na ziara ya Barack Obama mwezi Julai ni miongoni mwa ajenda ya mazungumzo katika kipindi chote hicho atakua nchini Kenya baada ya mwezi mmoja ya shambilio dhidi ya Chuo kikuu cha Garissa.

John Kerry amewasili Nairobi, mji mkuu wa Kenya Jumapili mchana Mei 3 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ambapo usalama umeimarishwa tangu Jumamosi. Mjini Nairobi, vizuizi vya barabarani vya polisi wiliwekwa kwa wingi.

Mazungumzo yamepangwa kufanyika pamoja na serikali, upinzani na vyama vya kiraia. Katika ajenda ya mazungumzo, suala la mapambano dhidi ya ugaidi na suala la wanamgambo wa kiislamu wa Al Shebab, mwezi mmoja baada ya shambulio dhidi ya Chuo kikuu cha Garissa, lakini pia uwekezaji wa kiuchumi katika muendelezo wa mkutano wa kileke kati ya Marekani na Afrika uliofanyika mjini Washington mwezi Agosti mwaka jana.

Ziara ya Rais Barack Obama, iliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Julai pia itajadiliwa. Maandalizi tayari yameanzishwa katika suala la usalama.

Ziara hii inatafasiriwa na vyombo vya habari vya Kenya kama kuboresha mahusiano katika ya nchi hizi mbili. Tangu uchaguzi wake wa kwanza mwaka 2008, Rais Obama alikuwa hajaweka mguu nchini Kenya, nchi alikozaliwa baba yake. Ziara ya mwisho ya ngazi kama hii ilifanyika mwaka 2012 na Hillary Clinton.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.