Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Zaidi ya watu 40 wauawa katikati mwa Nigeria

Watu wasiopungua 45 wameuawa katika shambulio lililoendeshwa dhidi ya jimbo la Bénoué, kusini mwa Abuja. Polisi ya jimbo la Bénoué inawashuku wafugaji kuwa ndio wamehusika na mauaji hayo. Uchunguzi umeanzishwa.

Foleni ya wakimbizi wa Nigeria wakisubiri kuteka maji katika kambi ya Minawao, kaskazini mwa Cameroon, Februari 18 mwaka 2015.
Foleni ya wakimbizi wa Nigeria wakisubiri kuteka maji katika kambi ya Minawao, kaskazini mwa Cameroon, Februari 18 mwaka 2015. REUTERS/Bate Felix Tabi Tabe
Matangazo ya kibiashara

Nigeria imekua ikishuhudia mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo, hususan mauaji yanayoendeshwa na kundi la Boko Haram.

Mauaji yamekua yakiripotiwa kila kukicha nchini Nigeria, hususan katika meneo ya vijiji, na katika maeneo kunako kusanyika halaiki ya watu ikiwa ni pamoja na sokoni, katika vituo vya basi na kadhalika.

Hivi karibuni majeshi ya Chad, Cameroon, Nigeria na Niger yalianzisha kwa pamoja operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram.

Hata hivyo kundi la Boko Haram bado limeendelea kushikilia maeneo kadhaa, kaskazini mwa Nigeria.

Kundi hili limekua likiendesha pia mashambulizi katika nchi jirani za Nigeria, ikiwa ni pamoja na Chad, Cameroon na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.