Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKOHARAM-MAMLUKI-USALAMA

Mamluki wa Afrika Kusini katika vita dhidi ya Boko Haram

Taarifa za kuwepo kwa mamluki wa Afrika Kusini nchini Nigeria zaonekana kuthibitishwa, wakati nchi hiyo ikiendelea kushuhudiwa mashambulizi ya Boko Haram.

Askari polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, Nigeria, katika operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni 2013.
Askari polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, Nigeria, katika operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni 2013. AFP PHOTO / Quentin Leboucher
Matangazo ya kibiashara

Uvumi wa kuwepo kwa mamluki hao ulianza kuzagaa tangu kuchapishwa kwenye mtandao wa Twitter picha inayoonesha mzungu akiwa amevalia magwanda ya kijeshi, huku akivalia pia fulana inayozuia risasi kuingia mwilini, akiwa katika gari la kijeshi akizunguka katika mitaa ya Maiduguri.

Hata hivyo taarifa ambazo zimeendelea kugonga vichwa vya habari nchini Nigeria, ni kuuawa kwa raia wa Afrika Kusini Jumatatu wiki hii kaskazini mashariki mwa Nigeria. Raia huyo alikua aliajiriwa na kampuni ya ulinzi ya kibinafsi kutoka Afrika Kusini.

Ni kwa mara ya kwanza mwanajeshi wa kimamluki anayeshiriki katika vita dhidi ya Boko Haram kuawa. Raia huyo anajulikana kwa jina la Leon Lotz, mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi. Gari alilokuwemo lililengwa wakati alipokua akizunguka katika jimbo la Borno, karibu na eneo linalodhibitiwa na Boko Haram.

Akihojiwa kuhusu tukio hilo, rais Goodluck Jonathan ameeleza kuwepo kwa kampuni mbili za ulinzi za kibinafsi kutoka Afrika Kusini katika ardhi ya Nigeria, akibaini kwamba kampuni hizo “ zimekua zikitoa walimu na mafundi” kwa jeshi. Rais wa Nigeria, hata hivyo, hakutaja majina yao, uraia wao au pia idadi yao.

Mamia wa mamluki wanasadikiwa kushiriki katika mapigano dhidi ya Boko Haram. Miongoni mwao ni pamoja na wanajeshi wa zamani wa jeshi la Afrika Kusini katika utawala wa ubaguzi wa rangi pamoja na wanajeshi kutoka Urusi ya zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.