Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-MAUAJI-USALAMA

Boko Haram yashambulia vijiji katika visiwa vya ziwa Chad

Niger imeshuhudia kwa mara nyingine shambulio la Boko Haram Jumapili Jioni. Wanamgambo wa Boko Haram waliendesha mashambulizi katika vijiji vilioko katika ziwa Chad.

Nchi nne zinachangia ziwa Chad : Chad, Cameroon, Niger na Nigeria.
Nchi nne zinachangia ziwa Chad : Chad, Cameroon, Niger na Nigeria. RFI/Sayouba Traoré
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo bado ni ya muda, lakini kwa mujibu wa mashahidi katika vijiji hivyo, watu tisa kwa uchache waliuawa.

Wanamgambo wa Boko Haram waliingia katika vijiji hivyo wakitumia mitumbwi kwenye saa mbili usiku Jumapili Machi 1, na kuanza kushambulia kwa risasi na vilipuzi katika nyumba mbalimbali za vijiji hivyo.

Katika kisiwa cha Kui Keleha, watu wawili waliuawa, na wengine walichomwa moto ndani ya nyumba zao, na wengine tena walikufa maji wakati walikua wakijaribu kuokoa nafsi zao, kama alivyothibitisha, El Adj Aboubacar, mbunge wa Bosso.

“ Walichoma moto watu tisa kwa wakati mmoja, na mtumbwi uliyokua ukiwasafirisha wanawake na watoto, ambao walikua wakijaribu kuokoa maisha yao ulizama majini. Wakti huu watu wanane walifariki", amesema El Adj Aboubacar.

Kwa uchache watu 19 walifariki baada ya shambulio lililoendeshwa katika vijiji vya Kui Kaleha na Toumbu Buka, visiwa ambavyo vinapatikana katika ziwa Chad kwenye mpaka na Nigeria. Eneo ambalo ni vigumu kutoa ulinzi.

Karibu na eneo hilo, kijiji cha Bosso kimekua kikishuhudiwa mara kwa mara mashambulizi ya hapa napale tangu Boko Haram Iliposhambulia kijiji hicho Februari 6 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.