Pata taarifa kuu
CAR-ANTIBALAKA-MATEKA-Usalama

Mateka wa Ufaransa aachiliwa huru

Claudia Priest, raia wa Ufaransa aliyetekwa nyara Jumatatu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, ameachiwa huru, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laureny Fabius, ametangaza.

Doria ya kikosi cha Ufaransa kinachoendesha operesheni Sangaris katika mji wa Bangui, Desemba 2014.
Doria ya kikosi cha Ufaransa kinachoendesha operesheni Sangaris katika mji wa Bangui, Desemba 2014. AFP PHOTO / PACOME PABANDJI
Matangazo ya kibiashara

Claudia Priest amekua akijihusisha na misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“ Ndugu yetu mwananchi, Claudia Priest, ambaye alitekwa nyara mwanzoni mwa jumahili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, yuko huru sasa. Ni furaha kubwa kwetu sote, na kwa wale walijitoa wahanga kwa kuhakikisha ndugu yetu huyoa anaachiwa huru”, Laurent Fabius amesema katika tangazo.

Katika tangazo hilo, Laurent Fabius amewashukuru wale wote waliochangia kwa kuachiliwa huru kwa raia huyo wa Ufaransa hasa viongozi wa kidini, hususan askofu mkuu wa Bangui, Dieudonné Nzapalainga, ambaye alienda kumtafuta mwenyewe mateka huyo wa Ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa za RFI, raia huyo wa Ufaransa kwa sasa yuko katika ubalozi wa Ufaransa mjini Bangui. Waziri wa mambo ya nje, Laurent Fabius, ameongea nae kwa simu. Mmoja kati ya maafisa waliokaribu na Waziri, ameiambia RFI kwamba Claudia Priest afya yake ni nzuri.

Claudia Priest, mwenye umri wa miaka 67, alikamatwa Jumatatu Januri 20 mwaka 2015 akiwa pamoja na mwenzake kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wanamgambo wa kundi la Anti-balaka ndio walihusika na utekaji nyara huo, wakidai achiliwe kiongozi wao Rodrigue Ngaïbona, maarufu “ jenerali Andjilo” , aliyekamatwa mwishoni mwa juma lililopita na kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, Minusca. Kiongozi huyo wa kivita wa Anti-balaka anazuiliwa mjini Bangui.

Haijajulikana hatma ya mateka mwengine aliyekua pamoja na Claudia Priest, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.