Pata taarifa kuu
UGANDA-MAREKANI-LRA-ICC

Ongwen, mkuu wa zamani wa LRA, atakabidhiwa Hague

Dominic Ongwen, mtu aliye karibu na Joseph Kony na Kamanda wa zamani LRA, atakabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ili ahukumiwe kwa makosa yanayomkabili ilikwa ni pamoja na uhalifu didi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita kwa uhalifu wa kivita.

Jeshi la Uganda likipiga doria katika msitu baada ya kuona nyayo za miguu ya wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA.
Jeshi la Uganda likipiga doria katika msitu baada ya kuona nyayo za miguu ya wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mikono mwa vikosi vya Marekani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kujisalimisha wiki moja iliyopita, Ongwen amelituikia karibu miaka 25 katika kundi la waasi wa Uganda la LRA.

Wakati huo huo maafisa wa serikali ya Uganda wamethibitisha kwamba kiongozi huyo wa juu wa kundi la waasi wa Uganda la LRA, atakabidhiwa kwa Mahakama ya kimataifa ya ICC.

Hata hivyo serikali ya Uganda imesema itaendelea kushauriana na Marikani kuhusu hali ya kamanda huyo wa LRA aliyekamatwa, Dominic Ongwen, huku jeshi la nchi hiyo likisema itakuwa bora iwapo atakabidhiwa kwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC.

Kamanda huyo ni miongoni mwa watu wa kundi la LRA wanaotafutwa na upande wa mashitaka katika Mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kosa la kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu katika maeneo kadhaa yalikuwa yakidhibitiwa na waasi hao.

Waasi wa Seleka walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako Dominic Ongwen alikamatwa walisema kuwa muasi huyo alikamatwa ingawa wanajeshi wa Marekani wanasema kuwa alijisalimisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.