Pata taarifa kuu
BURUNDI-CENI-MENUB-UCHAGUZI-MVUTANO-SIASA

Viongozi wasusia sherehe za uzinduzi wa Menub

Serikali ya Burundi imesusia sherehe za kuzinduliwa rasmi kwa ujumbe wa uangalizi wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi Mei na Juni nchini humo Menub wakati wasiwasi unaongezeka kuhusiana na hatari ya kutokea ghasia katika uchaguzi huo muhimu.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akihojiwa kuhusu kugombea muhula mwengine katika uchaguzi wa Urais..
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akihojiwa kuhusu kugombea muhula mwengine katika uchaguzi wa Urais.. AFP/ROBERTO SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo zilifanyaiak Jumatatu Januari 12 mwaka 2015 mjini Bujumbura.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini humo, Daniel Kabuto ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa kuna matatizo ya kiufundi yanayohusu jukumu la ujumbe huo, akisema hauna mamlaka ya kuchunguza na kuhakiki matokeo ya mwisho, kitu ambacho amesema kinaweza kufanywa tu na tume ya uchaguzi ya taifa, nchini humo Ceni.

Kabuto amesema ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuleta tume ya uangalizi na sio ya kuhakiki uchaguzi. Kwa upande wa serikali uhakiki wa matokeo ya uchaguzi ni kuiondolea wajibu wake tume ya  uchaguzi.

Marais wawili wa zamani, Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye, wawakilishi wa muungano wa vyama vya upinzani na mabalozi wa nchi za kigeni nio walishiriki sherehe za kuzindua rasmi shughuli ya ujumbe wa uangalizi wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya uchaguzinchini Burundi Menub.

Hayo yanajiri wakati mvutano bado unaendelea kati ya vyama vya kisiasa vya upinzani na tume huru ya uchaguzi. Vyama vya upinzani vinaendelea kuomba vikisisitiza kufanyika kwa mkutano utakaoongozwa na taasisi ya kidini ili kujadili kuhusu zoezi la kupiga kura lililomalizika mwaka jana na matokeo yake.

Wakati huo huo Viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani, pamoja na baadhi ya maaskofu wa Kanisa katoliki nchini Burundi wametoa misimamo yao kuhusu kugombea kwa muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Kwa upande wake askofu Simon Ntamwana, kiongozi wa Kanisa katolika mkoani Gitega, mji mkuu wa pili nchini Burundi, amesema kamwe hatounga mkono kugombea kwa rais Nkurunziza kwa muhula watutu, akimaanisha kuwa itakua kuwafanya raia watumwa wake.

Chama cha Cndd-Fdd, kupitia msemaji wake Onesime Nduwimana, kimebaini katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii kwamba muda wa kumchagua mgombea katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya chama hicho haujawadia.

Hata hivyo baadhi ya maseneta wazamani wa chama cha Cndd-Fdd wameanza kutoa misimamo yao kuhusu kugombea kwa ria Nkurunziza katika uchaguzi wa rais.

Seneta wa zamani kutoka chama hicho Richard Nimbesha amebaini kwamba rais Nkurunziza Katiba ya nchi haimruhusu rais Pierre Nkurunziza aidha marais wengine watakao kuja kugombea mihula mitatu, huku akimaanisha kuwa rais Nkurunziza amesha timiza mihula miwili katika uongozi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.