Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-UN-USALAMA

UN yanyooshea kidole kutumwa kwa majeshi ya Burundi DRC

RFI inaendelea kutathimini ripoti ya timu ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo itatolewa hivi karibuni.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wakemea kana kwamba Bujumbura haikutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa majeshi yake katika ardhi ya Congo.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wakemea kana kwamba Bujumbura haikutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa majeshi yake katika ardhi ya Congo. Getty Images/ Bobby Model
Matangazo ya kibiashara

Wataalam hao wanarejelea hatua iliyochukuliwa ya kupelekwa kwa majeshi ya Burundi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, taarifa ambayo imekanushwa mpaka sasa na serikali ya Burundi pamoja na Congo.

Ripoti hiyo imetoa vithibitisho vya kuwepo kwa vijana wa chama tawala nchini Burundi Cndd-Fdd (Imbonerakure) katika ardhi ya Congo.

Katika ripoti hiyo, wataalam wa Umoja wa Mataifa wamekemea kwamba serikali ya Bujumbura haikutoa taarifa yoyote kuhusu kuwepo kwa wanajeshi wake katika ardhi ya Congo aidha kutoa msaada kwa jeshi la Congo FARDC, wala kuingiza silaha nchini Kongo.

Hii inaelezwa na azimio 1807 la Umoja wa Mataifa juu ya vikwazo vya silaha, hata kama serikali ya Congo itakua ilikubaliana na serikali ya Burundi kupelekwa kwa wanajeshi wa Burundi nchi mwake.

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa liliomba serikali ya Burundi mara kadhaa kutoa taarifa ya kuwepo kwa majeshi yake Congo, bila mafanikio. Ingawa kwa ombi la Kinshasa, askari wa Burundi waliondoka nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.