Pata taarifa kuu

Baadhi ya wachambuzi hawana imani na kusitishwa kwa uhalifu wa LRA

Siku kadhaa zikiwa zimepita toka serikali ya Marekani na Uganda zithibitishe kujisalimisha kwa ofisa mmoja wa juu wa kijeshi wa kundi la waasi wa Uganda wa Lords Resistance Army – LRA, wachambuzi wa mambo bado hawaoni kama vita dhidi ya kundi hili imetamatika.

Picha ya zamani ya Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wa juu wa kundi la waasi wa Uganda LRA.
Picha ya zamani ya Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wa juu wa kundi la waasi wa Uganda LRA. ushahidi.universaljurisdiction.org
Matangazo ya kibiashara

Juma hili, Domminic Ongwen mmoja wa watu wanaotajwa kuwa ni mtu wa karibu wa kiongozi wa kundi hilo, Joseph Kony, alijisalimisha kwa wanajeshi wa Marekani walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, hatua iliyoshangaza wengi.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa licha ya kuendelea kujisalimisha kwa baadhi ya maofisa wa juu wa kundi hilo, bado vita dhidi ya LRA havijaisha.

Wachambuzi hao wamebaini kwamba huenda serikali ya Uganda inasaka msaada na uungwaji mkono na Jumuiya ya kimataifa kutokana na harakati zake za kukabiliana na LRA, kundi ambalo huenda likawa linafikia ukingoni na harakati zake.

Kundi la zamani la waasi wa Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati lilibaini hivi karibuni kwamba, Ongwen, hakujisalimisha bali alikamatwa na wapiganaji wa kundi hilo, na kulitaarifu jeshi la Marekani siku taatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa juu wa kundi la LRA, akiwa pia mshirika wa karibu wa Joseph Kony.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.