Pata taarifa kuu
CAR-ANTIBALAKA-Machafuko-Usalama

Machafuko yashuhudiwa kusini magharibi mwa CAR

Miji pamoja na vijiji kadhaa kusini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati vinakabiliwa wakati huu na wimbi la machafuko, baada ya hali hiyo kushuhudiwa miezi iliyopita katikati ya nchi hiyo.

Matukio hayo ambayo yamesababisha maafa makubwa yametokana na kukamatwa kwa mwanamgambo mmoja wa kundi la Anti-balaka katika mji wa Carnot,kaskazini mwa mkoa wa Mambéré-Kadéï, nchini Jmhuri ya Afrika ya Kati
Matukio hayo ambayo yamesababisha maafa makubwa yametokana na kukamatwa kwa mwanamgambo mmoja wa kundi la Anti-balaka katika mji wa Carnot,kaskazini mwa mkoa wa Mambéré-Kadéï, nchini Jmhuri ya Afrika ya Kati REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi na mapigano vimesababisha vifo vya mamia ya raia, ambao wengi wao ni raia wa kawaida. Milio ya risasi imekua ikisikika hadi usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 24 katika mji wa Carnot.

Hali ya wasi wasi inaripotiwa katika mkoa wa Mambéré-Kadéï, kusini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka na Cameroon.

Hata hivyo watu wanane ikiwa ni pamoja na wanawake wawili na wanaume sita waliuawa katika shambulio lililoendeshwa Jumanne Desemba 23 katika vijiji vya Bombo na Tanga. Taarifa hiyo imethibitishwa na mkuu wa manispa ya jiji la Gamboula, kilomita zaidi ya sitini na vijiji hivyo.

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja tawala, wauaji hao wamekua wakitokea nchini Cameroon, ambayo inatazamiwa kuwatuma askari wake kulinda eneo hilo.

Katika mji wa Canot miliyo ya risasi ilisikika mchana kutwa Jumanne Desemba 23 hadi usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 24 milio ya risasi imekua ikisikika.

Matukio hayo ambayo yamesababisha maafa makubwa yametokana na kukamatwa kwa mwanamgambo mmoja wa kundi la Anti-balaka katika mji huo wa kaskazini mwa mkoa wa Mambéré-Kadéï. Visa vya uporaji vilishuhudiwa katika mji huo, huku milio ya risasi ikiendelea kusikika usiku kucha.

Hayo yanajiri wakati amabpo watu kumi wanasadikiwa kuuawa katika mji wa Nola. Watu hao wmeuawa na watu kutoka jamii ya Peul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.